Sheria na Masharti

1. MAELEKEZO

Mtoa Huduma alinipatia taarifa katika utafiti wa mchujo na kubainisha wasifu ikielezea namna ambavyo utafiti utafanywa.

Ninakubali kufuata maelekezo yote yaliyotolewa kwenye utafiti wa mchujo na kubainisha wasifu ili niweze kutoa maoni yangu kuhusu kusudi la utafiti (kushiriki katika utafiti wa ana kwa ana moja kwa moja mtandaoni).

Mtoa huduma Human8 amepewa jukumu hili na mfadhili ambaye jina lake litatajwa mwishoni mwa utafiti huu.

2. PICHA, VIDEO

Ninakubali kupigwa picha, kuchukuliwa video, kuchunguzwa na kuulizwa maswali na Mtoa Huduma na/au Mfadhili katika mawanda ya ushiriki wangu kwenye utafiti, ama mtu binafsi au katika kundi ikiwa ni pamoja na katika mahojiano.

Aidha, ikiwa Utafiti utahitaji hivyo, ninakubali kuchapisha maoni, video, na/au picha zangu kwenye intaneti ambazo zitahusianishwa na mimi. Ikiwa kutatokea mkanganyiko kati ya hati hii na Masharti ya Jumla kwa ajili ya Matumizi ya jukwaa hilo, Masharti ya Jumla yatatumika.

Ninampa Mfadhili haki ya kutumia picha yangu kama ilivyopigwa katika nia mbalimbali katika kipindi chote cha Utafiti. Neno “Picha” hujumuisha picha zozote mjongeo au mnato vilevile sauti yangu kama ilivyorekodiwa katika kipindi chote cha Utafiti. Mfadhili anaidhinishwa kuongeza, kutumia, kuhariri, kufuta, kuunda upya, kuchakata na kuingiza sauti (kwa makusudi ya tafsiri, n.k) Picha yangu ya awali vyovyote vile wanavyoona inafaa.

Ninatoa idhini kwa Mfadhili kutumia picha yangu:

  • kwa ajili ya matumizi yote ya ndani ya ofisi (utafiti, mawasiliano, nk.)
  • kwa ajili ya mawasilisho ya kielimu ya ndani na nje ya ofisi, na kwa namna yoyoye kwa makusudi yasiyokuwa ya kibiashara.

Vyovyote vile picha yangu inavyotumika, Mfadhili atahakikisha kwamba hakuna uhusiano kati ya jina langu na picha yangu.

Idhini hii inatolewa bila kufidiwa malipo yoyote, duniani kote, kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia mwishoni mwa utafiti bila kikomo kuhusu idadi ya nakala au aina ya njia ya kuhifadhia iwe aina hiyo inajulikana wakati wa kusaini au la.

Nina haki ya kuondoa idhini hii wakati wowote kwa taarifa ya maandishi iliyotumwa na mtumaji aliyesajiliwa kwenda kwa Mtoa Huduma.

3. TAARIFA BINAFSI

Ninakubali waziwazi kuruhusu data zangu binafsi (kama vile jina la kwanza, jina la mwisho, anwani, aina ya nywele, na aina ya ngozi) zikusanywe na kuchakatwa na Human8.

Ninakubali kumruhusu Mfadhili apokee na kuchakata taarifa za utafiti zinazohusiana na mimi, kuondoa jina langu la kwanza na la mwisho na anwani.

Ninajua kwamba itatumiwa kwa ajili ya makusudi yafuatayo:

  • Kuboresha ufahamu kuhusu mahitaji ya walaji na vile wanavyofanya mambo
  • Kuanzisha kanzi data ya maarifa kuhusu Bidhaa hizi

Taarifa zangu binafsi hazitatumiwa kwa makusudi mengine yoyote bila idhini yangu ya maandishi. Itahifadhiwa na Mtoa Huduma/Mfadhili kwa miaka 3 kuanzia mwisho wa utafiti (ingawa kipindi hiki kinaweza kuongezwa kwa utekelezaji wa kifungu cha sheria).

Kulingana na Sheria, nina haki ya kufikia, haki ya kurekebisha, haki ya kuhamisha data, na haki ya kufuta taarifa zangu Pia ninaweza kupinga taarifa zangu zisichakatwe. Ili kutumia haki zangu, ni lazima nitume ombi langu kwenda kwa Mtoa Huduma wa Utafiti: Human8 (platformsupport@wearehuman8.com, Evergemsesteenweg, 195, 9032 Wondelgem, Belgium). Ikiwa baada ya kuwasiliana na Mtoa Huduma kisha nikaamini kwamba haki zangu hazikuheshimiwa, ninaweza kuwasilisha madai yangu mtandaoni kwenda “Mamlaka ya Ulinzi wa Data” ya Ubelgiji, (anwani) Drukpersstraat 35, 1000 Brussel, (simu) 32 (0)2 274 48 00, (barua pepe) contact@apd-gba.be.

Ikiwa sheria itahitaji hivyo, zitatumwa kwenye mamlaka ya Ufaransa au mamlaka ya afya ya ughaibuni chini ya masharti yanayohakikisha kuna usiri. Aidha, watoa huduma (kama vile watoa huduma wa TEHEMA au huduma za uchanganuzi wa picha), baadhi yao watakuwa nje ya Umoja wa Ulaya ua katika nchi ambapo data yangu ilikusanywa, wanaweza kuwa na idhini ya kufikia taarifa zangu binafsi kwa makusudi ya utafiti, au matengenezo ya kiufundi, pamoja na mengine. Mwisho, ili kulinganisha na kuwa na uzoefu bora wa ukusanyaji data katika muktadha wa Utafiti, zinaweza kutumwa kwa makampuni yanayohusiana na Mfadhili au matawi yake katika nchi nyingine duniani kote.

4. KULINDA TAARIFA ZILIZOKUSANYWA

Kufikia taarifa zangu nyakati zote zitafikiwa na watu walioidhinishwa tu, ambao watadumisha usiri wake.

Mtoa Huduma na Mfadhili watahakikisha kwamba kiwango cha ulinzi wa taarifa zangu binafsi hufuata sheria husika za ulinzi wa taarifa binafsi na kiwango hicho ni sawa na kile kinachohitajika ndani ya Umoja wa Ulaya.

5. USIRI

Katika utafiti wote na kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia mwishoni mwa utafiti, Ninakubali kutofichua, kunakili, au kutumia taarifa yoyote kuhusu utafiti huo, ambayo ninaweza kuwa nimeijua katika kipindi cha Utafiti. Ninakubali kutoshiriki na mtu yeyote hati zozote nilizo nazo kuhusu utafiti na kuziharibu haraka bila kujali zimehifadhiwa katika kifaa gani (yaani, karatasi, picha, video, n.k.).

6. MAONI & MAPENDEKEZO

Ninaelewa kwamba ninaweza kuulizwa kutoa mapendekezo kuhusu bidhaa mpya, vifaa, na.au huduma katika tasnia ya vipodozi na urembo na kutoa maoni kuhusu bidhaa na/au huduma ambazo zitawasilishwa. Ninampatia Mfadhili haki zote za ubunifu kuhusu mapendekezo na maoni yangu. Kwa hiyo mmiliki atakuwa na umiliki kamili wa Mapendekezo na Maoni bila mipaka ya aina yoyote.

7. KUJIONDOA KWENYE UTAFITI

Kushiriki kwenye utafiti ni hiari, na ninaelewa kwamba ninaweza kukataa kushiriki au ninaweza kujiondoa muda wowote Pia ninaelewa kwamba kushiriki kwangu kunaweza kuingiliwa wakati wowote bila kutoa ukubali wangu kwa Mtoa Huduma au Mfadhili.

8. FIDIA

Kama ilivyoelezwa kwenye utafiti wa mchujo na kubainisha wasifu, ninaelewa kwamba nitapokea malipo ili kufidia gharama za vikwazo vinavyohusiana na kushiriki kwenye Utafiti. Kiwango halisi na mtoaji wa malipo hayo utaambiwa wakati wa kuanza utafiti. Ikiwa nitachagua kusitisha kufanya Utafiti au ikiwa Utafiti utaboreshwa, fidia itakokotolewa kulingana na nilivyoshiriki.

9. IDHINI

Kama sehemu ya utafiti huu, HUMAN8 kwa niaba ya mfadhili, itachakata taarifa zako binafsi ili kuelewa tabia na mitazamo ya watumiaji wa bidhaa za urembo na umuhimu wa urembo katika maisha yao.

Hii itafanywa kulingana na sheria kuhusu data binafsi. Taarifa zako zitabaki kuwa siri na zitahifadhiwa kwa kipindi kifupi, kwenye seva zetu salama, na zitahifadhiwa pamoja na majibu ya washiriki wengine.

Kulingana na Sheria ya Ulinzi wa Jumla wa Data n°2016/679 na Sheria ya Ulinzi wa Data ya Ufaransa ya Januari 6 1978, unahaki ya kufikia taarifa zako binafsi, kuziboresha au kuzifuta, kuomba ukomo wa wa uchakataji wa taarifa zako, au kupinga uchakataji huu.

Tunakutaarifu kwamba baadhi ya majibu ambayo yataombwa yanaweza kuchukuliwa kuwa ni taarifa nyeti ndani ya maana kwa mujibu wa sheria.

Kwa ombi lolote kuhusu uchakataji wa taarifa zako binafsi, utambulisho wa mfadhili, au kutumia haki zako, unaweza kuwasiliana na Afisa wa Ulinzi wa Data wa HUMAN8 kupitia anwani ifuatayo: dpo@wearehuman8.com.