SERA YA FIDIA

1. Ustahiki:

Fidia (kwa ujumla na mojamoja ‘Fidia’) hutolewa tu kwa watu ambao wamepokea mwaliko kutoka InSites Consulting na ni wakazi halali wa nchi waliyoionyesha kwenye utafiti, na ambao wana umri wa miaka 18 au zaidi wakati wa kuingia. Waajiriwa (na wanafamilia wao wa karibu au watu wanaoishi nyumbani) wa InSites Consulting na washirika wao, kampuni tanzu, na vitengo na makampuni na wagavi wanaohusiana vilevile mashirika yake ya matangazo, promosheni na kutoa maamuzi (kwa pamoja “Wahusika wa Fidia”) hawastahiki kushiriki au kushinda. Wanafamilia wa karibu humaanisha wazazi, wazazi wa kambo, watoto, watoto wa kambo, ndugu, ndugu wa kambo au wenzi, bila kujali wanaishi wapi. ‘Watu wanaoishi nyumbani’ humaanisha watu wanaokaa kwenye nyumba moja angalau miezi mitatu kwa mwaka, iwe wana uhusiano au la. Fidia zitatolewa kulingana na sheria na taratibu zinazotumika za serikali kuu, jimbo, mkoa na serikali za mitaa. Ushiriki unajumuisha mshiriki kukubali kikamilifu na bila masharti Kanuni Rasmi hizi na maamuzi ya InSites Consulting, ambayo ni ya mwisho na lazima yafuatwe katika masuala yote yanayohusiana na Fidia. Kupokea fidia kunatarajiwa baada ya kukidhi matakwa yote yaliyowekwa hapa. Batili pale ilipokatazwa.

2. Fidia

Utumikaji

Fidia inatolewa kwa mshiriki pale tu anapokuwa amekamilisha mahojiano ya video ambayo yatafanyika pamoja na mteja na/au mwongoza mjadala na/au mwakilishi wa InSite Consulting, ambayo yatapangwa wakati ambao unawafaa pande zote. Ni washiriki tu wenye wasifu unaokidhi sifa ndio wataalikwa kushiriki.

Ili upewe fidia, washiriki wote wanatarajiwa kujibu kwa uaminifu maswali yote wanayoulizwa wakati wa mahojiano. Ikiwa mteja na/au msimamizi wa mjadala na/au mwakilishi wa InSites Consulting wakati au baada ya mahojiano kukamilika ataamua kuwa ubora wa majibu ya mshiriki haukubaliki, wana uhuru kamili wa kuamua kutomlipa mshiriki fidia aliyokuwa ameambiwa hapo awali.
Ili kupokea fidia kamili ambayo itaelezwa kwa njia ya mawasiliano ya barua pepe, mshiriki anatarajiwa kushiriki katika mahojiano kwa urefu kamili ambao alielezwa.

Ikiwa mahojiano yatafupishwa, kwa zaidia ya asilimia 50 ya ilivyopangwa, kwa sababu za kiufundi au sababu nyingine ambazo zinapaswa kuwa chini ya udhibiti wa mshiriki na hazihusiani na mteja na/au msimamizi wa mjadala na/au mwakilishi wa InSites Consulting, mshiriki hatalipwa kiasi chochote cha fidia aliyoelezwa kuwa atapokea.

Aina ya fidia

Ukomboaji wa Fidia huweza kuwa katika mfumo wa vocha au kadi ya zawadi, au malipo kwenye akaunti ya PayPal au kadi nyingine mtandaoni: Tuna haki ya kubadilisha aina ya Fidia na kutoa Fidia nyingine yenye thamani sawa kwa busara yetu. Jumla ya thamani ya Motisha ni kulingana na viwango vya nchi mahususi na inaamuliwa na jitihada za wastani alizoombwa mshiriki. Thamani ya zawadi iliyoandaliwa kwa ajili ya ushiriki mkamilifu atajulishwa mshiriki kwa njia ya barua pepe. Fidia zitaisha muda wake ikiwa hazitakombolewa ndani ya miezi 24 baada ya kutolewa kwa mshiriki.

3. Hali ya Fidia

Washiriki wanakiri kwamba Fidia huenda zikazingatia sheria na masharti yaliyotolewa na washusika wengine na huenda zikaonyesha tarehe ya mwisho wa matumizi. Vocha/kadi za zawadi kwa kawaida zinaweza kutumiwa tu kwa ajili ya kununua bidhaa/huduma kulingana na masharti ya kampuni inayotoa hizo kadi za zawadi, zisirejeshwe, zisikombolewe kwa kuchukua fedha taslimu (isipokuwa kwa kiwango kinahohitajika na sheria) au kutumiwa kama malipo au kuwekwa kwenye akaunti yoyote ya kadi ya mkopo. Si halali kwa manunuzi ya awali. Vocha hazitabadilishwa ikiwa zitapotea au kuibiwa. Hakuna wakati ambapo thamani ya vocha itazidi thamani iliyotajwa. InSites Consulting haiwajibiki kwa matendo yoyote au kushindwa kufikia maagano kwa mshusika mwingine yeyote kwa kutowasilisha, kutotenda au matatizo katika Fidia au bidhaa/huduma zilizonunuliwa kwa kutumia Fidia. Wahusika wengine wanaotoa Fidia si wafadhili wa utafiti au mpango wa Fidia. Ikiwa itatokea mshiriki ananunua zaidi ya thamani iliyobainishwa, mshiriki atawajibika kabisa kwa malipo ya hizo gharama za zaida. Hakuna ubadilishaji wa fidia isipokuwa kama itaidhinishwa na InSites Consulting kwa busara yake. Fidia haihamishiki au kupewa mtu mwingine. Mshiriki anawajibikia ushuru na kodi zote zinazohusiana na upokeaji na/au utumiaji wa vocha. Fidia zitatolewa kulingana na sheria na taratibu zinazotumika za serikali kuu, jimbo, mkoa na serikali za mitaa. Kupokea Fidia kunategemea utimizaji wa matakwa yote yaliyowekwa hapa.

4. Masharti ya jumla

Uamuzi wa InSites Consulting kwa kuzingatia vipengele vyote vya Fidia ni wa mwisho na unapaswa kufuatwa na washiriki wote bila haki ya kukata rufaa, ikiwa ni pamoja na, si tu, uamuzi wowote kuhusu ustahiki/ kutofuzu kwa maingizo na/au washiriki. Jaribio lolote linalofanywa na mshiriki ili kupata fidia kwa kutumia barua pepe kadhaa, utambulisho, usajili na uingiaji kwenye akaunti, au njia nyingine yoyote, litabatilisha ushiriki wa mtu huyo; pia, mtu huyo ataondolewa katika kushiriki. Matumizi ya mfumo au huduma yoyote ya kiotomatiki ili kushiriki yanazuiwa na kufanya hivyo kutasababisha kuondolewa katika kushiriki. Ikiwa utatokea mzozo kuhusu usajili wowote, mtumiaji wa akaunti ya barua pepe hiyo iliyotumika kujisajili atachukuliwa kuwa ndiye mshiriki. ‘Mtumiaji wa akaunti’ ni mtu halisi ambaye amepewa anwani ya barua pepe na mtoa huduma ya Intaneti, mtoa huduma za mtandaoni au shirika lingine linalowajibika kutoa huduma ya anwani za barua pepe kwa vikoa vinavyohusiana na anwani zilizowasilishwa.

Vocha hazina thamani ya fedha taslimu na hazihamishiki. InSites Consulting haiwajibiki kwa upotevu, kucheleweshwa, kutokamilika, kutofaa, au majibu yaliyotumwa sehemu isiyo sahihi. Zawadi zinazingatia sheria zote zinazotumika za serikali kuu, mkoa na manisipaa. InSites Consulting haitawajibikia: (I) tovuti kushindwa kufanya kazi wakati wa shughuli; (ii) matatizo yoyote ya kiufundi au matatizo mengine yanayohusiana na mtandao wa simu au laini, mifumo ya kompyuta ya mtandaoni, seva, watoa huduma wa ufikiaji, zana au programu ya kompyuta; (iii) kushindwa kuwasilisha ingizo lolote au maelezo yoyote yanayopaswa kupokelewa, yaliyonaswa au kurekodiwa kwa sababu yoyote, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, matatizo ya kiufundi au msongamano wa shughuli kwenye intaneti au kwenye tovuti; (iv) jeraha au uharibifu wowote kwenye kompyuta ya mshiriki au mtu yeyote au vifaa vyovyote vinavyohusiana na au vilivyotokana na kushiriki katika shughuli; na/au (v) muunganiko wa yoyote kati ya hayo hapo juu.

InSites Consulting ina haki ya kuondoa, kurekebisha au kusitisha fidia (au kurekebisha Kanuni Rasmi hizi) kwa njia yoyote, ikiwa hitilafu itatokea, au tatizo la kiufundi, virusi vya kompyuta, hitilafu, kuchezea mfumo, kuingilia kati kusikoidhinishwa, udanganyifu, anguko la kiufundi au sababu nyingine yoyote iliyo nje ya uwezo wa InSite Consulting ambayo inaingilia utekelezaji sahihi wa mpango wa Fidia kama ilivyobainishwa na Kanuni Rasmi hizi. InSites Consulting (ikiwa inafaa), ina haki ya kughairi, kurekebisha au kusitisha fidia, au kurekebisha Kanuni Rasmi hizi kwa namna yoyote bila ilani ya mapema au kulazimika, ikiwa jambo lolote litatokea, hitilafu ya kuchapisha, kiuongozi au hitilafu nyingine ya aina yoyote, au kwa sababu nyingine yoyote ile. Bila kuweka mipaka ya ujumla wa haya yanayofuata, InSite Consulting ina haki ya kusimamia jaribio mbadala la ujuzi kadiri inavyoona inafaa kulingana na mazingira na/au kufuata sheria zinazotumika. InSites Consulting ina haki, kwa busara yake kabisa na bila ilani ya mapema, kurekebisha tarehe zozote na/au muda uliotajwa kwenye Kanuni Rasmi hizi, kwa kiwango ambacho ni cha lazima, kwa makusudi ya kuthibitisha uzingatiaji uliofanywa na mhusika au ingizo lolote kwa Kanuni Rasmi, au kama matokeo ya tatizo la kiufundi au tatizo lingine, au kwa kuzingatia mazingira yoyote yanayoathiri usimamizi mzuri wa fidia kama ilivyotajwa kwenye Kanuni Rasmi, au sababu nyingine yoyote.

Kwa kuingia kwenye tovuti, kila mshiriki anatoa idhini kwa InSites Consulting, wakala wake na/au wawakilishi kutunza, kushiriki na kutumia taarifa binafsi zilizowasilishwa pamoja na ingizo lao, taarifa za kujiandikisha na majibu ya shughuli kulingana na sheria na masharti.

5. Sheria inayoongoza na mizozo

Kanuni Rasmi na Fidia huongozwa na sheria za jumla za Ubelgiji na, kwa kila mshiriki, kwa sheria mahususi ya eneo la kisheria ndani ya nchi hiyo ambapo mshiriki huyo anaishi. Mahakama za kila mamlaka ya kisheria ya Ubelgiji itakuwa na mamlaka ya kisheria katika masuala yote na maswali kuhusu ujenzi, uhalali, tafsiri na utekelezekaji wa Kanuni Rasmi za Fidia, au haki na wajibu wa mshiriki na InSites Consulting kuhusiana na Fidia.

Masuala na maswali yote kuhusu ujenzi, uhalali, tafsiri na utekelezekaji wa kanuni rasmi au haki na wajibu wa mshiriki au InSite Consulting kuhusu fidia yataongozwa na kutafsiri kulingana na sheria za ndani za Ubelgiji bila kuathiri uchaguzi wowote wa sheria ya mgogoro wa kanuni za sheria au vifungu ambavyo vinaweza kusababisha matumizi ya sheria za nchi nyingine yoyote.

Fidia na migogoro yoyote inayoibuka chini yake au inayohusiana nayo itasimamiwa na sheria husika za Ubelgiji na mahakama husika za Ubelgiji zitakuwa na mamlaka kamili ya kisheria kusikiliza mzozo wowote au madai yanayotokea kuhusuana na Fidia au Kanuni Rasmi.